Mkutano Mkuu wa Mwaka unafanyika mara moja kila mwaka. Mkutano huu ni lazima ufanyike ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya kufunga mahesabu 9
kulingana na sheria Na 6. ya vyama vya Ushirika ya mwaka 2013, vinginevyo ni lazima kuomba kibali cha Mrajis.
Mambo yatakayojadiliwa ni:
(a) Kusoma/ kuthibitisha mambo ya Mkutano Mkuu wa Mwaka uliopita na yatokanayo;
(b) Kusoma, kupokea na kujadili Taarifa ya mkaguzi wa mahesabu na mizania;
(c) Mgao wa ziada (dividends) kama upo
(d) Kufikiria Tuzo kwa wajumbe wa Bodi na wengineo;
(e) Kuidhinisha Makisio ya Mapato na Matumizi ya Chama kwa mwaka unaofuata;
(f) Kuweka ukomo wa madeni
(g) Kuthibitishwa kuingizwa na /au kufukuzwa kwa mwanachama.
(h) Kupokea na kujadili Taarifa ya Bodi Muda wa tangazo la mkutano mkuu wa mwaka ni siku ishirini na moja (21) kabla ya siku ya mkutano.