TAARIFA YA FEDHA (BAJETI)

Taarifa ya mapato na matumizi inaandaliwa na kupelekwa katika Mkutano Mkuu wa mwaka kujadiliwa na Wanachama na kupitishwa na Wanachama kisha kupelekwa kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika kuidhinishwa.

MTIRIRIKO WA HESABU.

Vitabu vinavyotumika;

(a) Mapokezi;- – Stakabadhi za fedha.
(b) Malipo;

  • Hati za malipo.
  •  Hundi.
  •  Fedha kichele (petty cash).

(c) Daftari la fedha:

  • Kutambua mapokezi na malipo yanayofanyika.

(d) Leja kuu:

  • Kupokea miamala kutoka daftari la fedha na Jono stet.

(e) Urari:

  •  Kupokea muhtasari wa miamala kutoka leja kuu.

(f) Baada ya hapo utayarishaji wa hesabu za Chama hufanyika.

  • Daftari la mali za kudumu kutambua mali zinazomilikiwa na Chama kwa kuonyesha:-
  •  Tarehe ya ununuzi, jina la mali, thamani za mali, muuzaji wa mali, uchakavu wa mali, Baki halisi ya mali, hali ya mali, mahali mali zilipo, namba za utambulisho n.k.
  • Daftari la Wanachama:
  •  Kuonyesha kumbukumbu za Wanachama. Jina la Mwanachama tarehe ya kujiunga, jina mrithi, kazi ya mrithi, idadi ya Hisa n.k.

TAARIFA ZA FEDHA.

(a) Taarifa ya Bodi – Directors Report.
(b) Mizania – Balance Sheet.
(c) Mapato na matumizi – Income & exp account.
(d) Mabadiliko ya mtaji – Statement of changes in equity.
(e) Mtiririko wa fedha – Cashflow Statement.
(f) Maelezo ya ufafanuzi – Notes to the account.
(g) Majedwali mbalimbali – Schedules to the accounts.

AKAUNTI ZINAZOMILIKIWA NA CHAMA BENKI

1. CRDB
2. DAR ES SALAAM COMMERICAL BANK

NYARAKA MBALIMBALI ZINAOTUMILA KATIKA CHAMA

(a) Kadi za wadaiwa na wadai.
(b)Hati za madai kwa wadaiwa (barua)
(c) Hati za kudaiwa na watoa huduma (barua).
(d)Hati miliki za mali za Chama – ardhi na majengo.