Mkutano Mkuu Maalum tangazo lake ni siku saba (7)
Agenda ya Mkutano Mkuu Maalumu ni moja tu.
(a) Kutakuwa na Mkutano Mkuu Maalum wakati wowote iwapo utaitishwa na Bodi, Mrajis wa vyama vya Ushirika au kwa maombi ya maandishi ya Wanachama wasiopungua theluthi moja (1/3).
(b) Kwa Mkutano Mkuu Maalum ulioombwa na Wanachama, maombi lazima yataje sababu za kutaka mkutano huo ufanyike na waombaji lazima waandike majina yao kwa kirefu na yanayosomeka vizuri, namba zao za Uanachama na waweke saini zao katika barua ya maombi na kupeleka kwa Mwenyekiti wa Chama na nakala kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika;
(c) Mkutano Mkuu Maalum hautazungumzia jambo zaidi ya lile lililokusudiwa kuzungumziwa katika Mkutano huo.
Mikutano ya Bodi inafanyika mara sita kwa mwaka iliyoidhinishwa katika Bajeti ya Chama. Hata hivyo Bodi haizuiliwi kufanya mikutano zaidi ya sita kwa mwaka
isipokuwa mikutano hii zaidi ya sita Wajumbe hawatalipwa posho.