MKUTANO MKUU WA KAWAIDA

Mkutano Mkuu wa Kawaida tangazo lake ni siku ishirini na moja (21) Agenda zake ni:-

(a) Kusoma/kuthibitisha mambo ya Mkutano Mkuu wa Kawaida uliopita;
(b) Kuzungumzia na kuidhinisha mambo yote yahusuyo maendeleo ya Chama;
(c) Kufanya mabadiliko ya masharti ikibidi;
(d) Kuamua idadi ya wajumbe wa Bodi;
(e) Kununua na kuuza mali zinazohamishika na zisizohamishika;
(f) Kujadili na kutekeleza tafsiri na utekelezaji wa Sheria za Ushirika;
(g) Kuidhinisha makubaliano na mikataba;
(h) Iwapo haikuwezekana kufanyika Mkutano Mkuu wa Kawaida, Dondoo za Mkutano Mkuu wa kawaida zinaweza zikajadiliwa kwa pamoja na Dondoo za Mkutano Mkuu wa Mwaka;
(j) kuchagua au kusimamisha Wajumbe wa Bodi.