UWEKEZAJI

Taarifa Kuhusu Kiwanja Na. 702 Kitalu 46 – Kijitonyama, DSM (Mradi wa Kutafuta Mwekezaji)

  1. Aina ya Ubia
    • Ubia utakaowezesha mwekezaji kujenga jengo, kuendesha kwa kipindi kilichokubalika, na hatimaye kurejesha jengo kwa Chama (Mwenge Housing Cooperative Society – MHCS Ltd).
  2. Maelezo ya Kiwanja
    • Kiwanja Na. 702 Kitalu 46 kina ukubwa wa mita za mraba 4,750 na kinamilikiwa na Chama cha Ushirika cha Ujenzi wa Nyumba Mwenge kupitia hati Na. 101932.
    • Matumizi ya kiwanja hiki ni kwa ajili ya Community Centre.
    • Thamani ya Kiwanja: TZS 5,320,000,000 kwa bei ya soko.
  3. Hati ya Kiwanja
    • Hati ya umiliki ni ya miaka 99, ilitolewa tarehe 02/06/2007

Uwanja wa Michezo Na. 127 Kitalu Q Kibiki – Chalinze

  • Ukubwa: Hekta 1.25.
  • Mradi: Chama kinatafuta mwekezaji wa kujenga uwanja huu kwa kuweka nyasi, kuzungushia ukuta, kujenga sehemu za watu kukaa, na kufunga mageti.
  • Utaratibu wa Gharama na Mapato:
    • Gharama za mwekezaji zitarejeshwa katika muda uliopangwa na kukubalika na pande zote mbili (MHCS Ltd na mwekezaji).
    • Mapato yatakayopatikana kutoka uwanja huu yatagawanywa kati ya mwekezaji na MHCS Ltd kwa asilimia fulani kama makubaliano yatakavyoeleza.
    • Baada ya mwekezaji kurejesha gharama zake, uwanja utabaki kuwa mali ya Chama MHCS Ltd kwa asilimia mia moja.

Viwanja kwa Ajili ya Kujenga Hoteli

    • Kiwanja Namba 124 Kitalu Q Kibiki Chalinze chenye ukubwa wa mita za mraba 8897.
    • Kiwanja Namba 43 Kitalu Q Kibiki Chalinze chenye ukubwa wa mita za mraba 5827.
    • Kiwanja kwa ajili ya matumizi ya Community Centre chenye ukubwa wa mita za mraba 7767.
    • Kiwanja kwa ajili ya matumizi Shule ya awali – (Chekechea) chenye ukubwa wa mita za mraba 3984.

Uwekezaji katika viwanja hivi ni kwa ubia kati ya Mwekezaji na Chama MHCS Ltd ndani ya kipindi kitakachokubalika na pande zote. Baada ya Mwekezaji kurejesha gharama zake miradi inabaki katika Chama kwa asilimia mia moja (100%).

    • Miradi tarajiwa ni ununuzi wa ardhi katika mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kupima viwanja vya matumizi mbalimbali.

HISA

  • Chama kimewekeza Hisa elfu kumi (10,000) zenye thamani ya milioni tano (5,000,000) katika Benki ya Ushirika (KBCL).
  • Hisa TFC zenye thamani ya Tsh. 4,250,000/=

NYUMBA ZA MAKAZI – (Mradi uliokamilika)

Chama – MHCS Ltd kilisajiliwa rasmi tarehe 29.6.1971. nyumba zilijengwa katika Kitalu 43 Mwenge Dar Es Salaam. Nyumba zote za Wanachama zilijengwa za aina moja (100%).

Thamani ya nyumba moja ilikuwa Tsh. Elfu kumi na tano (15,000).