UONGOZI – (WAJUMBE WA BODI)

wajumbe wa bodi

(i) Dira

Dira ya Chama cha Ushirika wa Ujenzi wa Nyumba Mwenge ni kuwa taasisi bora ya Ushirika wa Ujenzi wa Nyumba na uwekezaji katika rasilimali zake. Lengo kuu ni kuendelea kujiimarisha kiuchumi na kutoa huduma kwa wanachama sambamba na kuendeleza falsafa ya kujitangaza kitaifa na kimataifa.

(ii) Dhima

Dhima kuu ya Chama cha Ushirika wa Ujenzi wa Nyumba Mwenge ni kuendelea kutafuta maeneo mapya ya ardhi, kuyamiliki, kuyapima, na kugawa viwanja kwa wanachama. Pia, chama kinajikita katika kutafuta vifaa vya ujenzi wa nyumba kwa wanachama na kuwaelimisha namna ya kutumia vifaa hivyo kwa busara ili kuwajengea uwezo mkubwa wa kiuchumi na maisha bora.